Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imeyataka makampuni ya simu za
mkononi Tanzania kuhakikisha yanaanza rasmi mpango wa punguzo la bei ya kupiga
simu katika mitandao mingine kutoka bei inayotumika sasa hivi ya shilingi 113
kwa dakika mpaka shilingi 34 na senti 92 ikiwa ni bei mpya inayotakiwa kuanza
kutumika kuanzia siku ya kwanza ya mwezi March 2013.
Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA Profesa John Nkoma amesema uamuzi wa kufanya
hivyo ni kutokana na kupanda kwa gharama za maisha ambapo makampuni hayo
yanatakiwa kuanza utekelezaji wa agizo hilo na hatua za kisheria zitachukuliwa
kwa kampuni yeyote ambayo itafanya kinyume na hayo maagizo.
Namkariri akisema “bei itaendelea kushuka kadri miaka inavyokwenda,
tarehe 1 january 2014 bei itatakiwa kuwa sh 32 na senti 40, tarehe 1 january
2015 sh 30 na senti 58, tarehe 1 january 2016
itatakiwa kuwa sh 28 na senti 57, hizi bei ni za juu kabisa na Kampuni za simu
ni ruksa kwao kuzungumza na wakatumia bei ya chini kabisa”
0 COMMENTS:
Post a Comment