Baada ya minongono mingi kuhusiana na hali ya msanii
mwenzao Vengu, hatimaye memba wa kundi ya Ze Orijino Komedy Masanja
mkandamizaji amefunguka na kueleza kuwa msanii mwenzao Joseph Shamba aka Vengu anaendelea vizuri baada ya kurejea kutoka India alikokuwa akitibiwa.
akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook leo Masanja
amesema kuwa Vengu bado anaendelea kupata matibabu akiwa nyumbani
“Ukweli ni kwamba Ndugu yetu Joseph Shamba (Vengu) yuko nyumbani
akiendelea na matibabu yake na uangalizi wa mara kwa mara kwa madaktari
baada ya kurejea kutoka India.” alisema masanja na kuongeza “…Muda
mwingi tuko naye na tunazidi kumuombea apone na arejee kutoa burudani.
Na mnaomuombea mabaya na kumzushia habari za kila aina tunawakabidhi kwa
Mungu awajalie busara.”
Habari hizi zimekuja wakati mzuri kwani habari za
kuugua na ugonjwa wa Vengu upatikanaji wake si wa wazi licha ya
mashabiki na jamii kufahamu kuwa Vengu anaumwa basi.
Tunamuombea mwenyezi Mungu amjalie mja wake aweze kupona na kurejea kazini kulitumikia taifa na jamii kwa ujumla.
0 COMMENTS:
Post a Comment