Picha
hii haina uhusiano na mmea wa Mvunge, tahadhari usije kuthubutu kuona
vitunda kama hivi na kuanza kuvitumia ukijua ndio dawa yenyewe.
Kwa
kutumia mabango, lengo likiwa kutangaza kazi zao, waganga
wengi wa tiba
asilia wamekuwa wakijinadi kuwa wanatoa tiba ya kurefusha maumbile ya
siri ya wanaume, kukuza makalio au matiti.Kushamiri
kwa mabando ya matangazo hayo kunatafsiriwa kwamba ni kutokana na
uhitaji mkubwa wa huduma hiyo nchini, huku watoa huduma husika
wakinufaika kwa kujikusanyia kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa
wahitaji.
Pia dawa zinazodaiwa kukuza makalio maarufu kama ‘mchina’, zimekuwa gumzo baada ya kuingia nchini, huku zikielezwa kukosa ubora na kwamba zina madhara makubwa. Lakini, taarifa mpya zinautaja mti wa Mvunge kuwa na uwezo wa kukuza makalio, matiti na kurefusha uume.
Pia dawa zinazodaiwa kukuza makalio maarufu kama ‘mchina’, zimekuwa gumzo baada ya kuingia nchini, huku zikielezwa kukosa ubora na kwamba zina madhara makubwa. Lakini, taarifa mpya zinautaja mti wa Mvunge kuwa na uwezo wa kukuza makalio, matiti na kurefusha uume.
Kaimu Msajili wa Tiba Asili na
Tiba Mbadala nchini, Dk Naomi Mpemba anasema kuwa mmea huo ambao huwa ni
mti mkubwa upo na kwamba una uwezo mkubwa wa kukuza maumbile hayo.
Anabainisha kuwa mmea huo ambao
hukua na kuwa mti mkubwa huzaa matunda yanayotumika kama dawa na
unapatikana wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, Pwani, Mbeya, Morogoro na
baadhi ya mikoa nchini:
Tulifuatilia na kutambua kuwa mti huo upo maeneo hayo na unatumiwa zaidi na waganga, hata picha za mti huo tunazo…
Jina jingine unaitwa Miegeya, mara nyingi unastawi katika maeneo yenye ardhi ya unyevunyevu, una tabia ya kustawi kama Mwembe na matunda yake huonekana kufanana na Mbuyu.
Hata hivyo, anasema kuwa asilimia kubwa ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala wanaotumia dawa hiyo ni wale wasiokuwa na usajili kutoka baraza hilo, hivyo kufanya huduma hizo kinyume cha utaratibu. Dk Mpemba anasema:
Kwa mujibu wa masharti yaliyopo katika agizo la Serikali kwa waganga hao, miiko, maadili na utendaji wa kazi zao umeelekeza kuwepo na usiri na kuaminiwa, kwa hiyo sisi tunaamini wanaojitangaza kutibu mambo hayo ni matapeli.
0 COMMENTS:
Post a Comment