Gazeti
la Sunday Mail la Uganda limeripoti kwamba Polisi wa nchi hiyo
wanaendesha uchunguzi ambapo huenda wakamfungulia mashitaka ya mauaji
mwanamuziki Joseph Mayanja, mke wake Daniella na kundi la muziki la Leon
Island.
Ni kutokana na kifo cha Robert Karamagi (27) aliyefariki katika
Hospitali ya Mulago baada ya majeraha aliyoyapata nyumbani kwa
mwanamuziki huyo huko Seguku Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kajjansi
Ibrahim Saiga alisema wamechukua ushahidi mbalimbali kutoka kwa majirani
na mashuhuda walioona, ushahidi ambao unapingana na ule uliotolewa na
familia ya Mayanja.
Huyu ndio mwizi mwenyewe ambae anadai hakujichoma mwenyewe bali kina Chameleone ndio walimchoma.
Huyu ndio mwizi mwenyewe ambae anadai hakujichoma mwenyewe bali kina Chameleone ndio walimchoma.
Pamoja
na kusema faili la uchunguzi huo litapelekwa kwa Mwendesha Mashitaka wa
Serikali (DPP) kwa ushauri, Saiga alisema pia baba wa Karamagi alikana
kwamba mwanaye alijimwagia mafuta na kujiwasha moto, pia alisema
mwanaye alipomwita hospitalini alimwambia aliteswa, akafungwa kamba,
akamwagiwa mafuta na kuchomwa moto na mwanamuziki huyo pamoja na wenzake
wa kundi lake.
Jose
Chameleone akihojiwa na NTV Uganda na kusema kwamba hilo swala
wameliacha kwenye mikono ya polisi, gazeti la sunday mail limeripoti pia
kwamba alhamisi iliyopita Jose Chameleone alihojiwa na wapelelezi kwa
muda mrefu lakini aliachiwa kwa dhamana.
0 COMMENTS:
Post a Comment