WAIGIZAJI ‘the big names’ wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na
Jacob Steven ‘JB’ wamezua minong’ono baada ya kugandana kimahaba hadi
wakawakera maustadhi, Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri katika Kijiji
Cha Kwadelo wilayani Kondoa, Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo
mastaa hao walikwenda kuzindua mpango wa Kilimo Kwanza, Ajira kwa Vijana
ulioongozwa na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati.
Waigizaji hao walionekana kupeana ‘kampani’ kwa kila walichokifanya, huku kila mmoja akigandisha mkono kiunoni kwa mwenzake na kushikanashikana hadharani huku Wema akideka na ‘kale kasauti kake kanakoweza kumtoa nyoka haraka pangoni’.

Baada ya uzinduzi kufanyika mashambani na kila mmoja kutoa neno la
kuhamasisha vijana kujiajiri kupitia kilimo, wasanii hao waliendelea
kugandiana, jambo lililosababisha maustadhi kuendelea ‘kuwamaindi’ kabla
ya kusoma dua na kuagana ambapo JB alimbeba Wema na kumpakiza kwenye
gari lao aina ya Toyota Noah, wakaelekea kwenye gesti waliyofikia
kijijini hapo tayari kwa kuendelea na ratiba nyingine.
Katika safari hiyo, mastaa hao waliambatana na wenzao wanaounda Bongo Movie Unity, Irene Uwoya, Single Mtambalike ‘Richie’ na Vincent Kigosi ‘Ray’.
Katika safari hiyo, mastaa hao waliambatana na wenzao wanaounda Bongo Movie Unity, Irene Uwoya, Single Mtambalike ‘Richie’ na Vincent Kigosi ‘Ray’.
0 COMMENTS:
Post a Comment