December 10, 2012

UZINDUZI WA CLUB MPYA INAYOITWA 327

Hi | 1:22:00 AM | | | | | | | |
 Wapenda burudani wa jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii wamesherekea uzinduzi wa Club mpya inayojulikana kama 327, iliyopo mitaa ya Mikocheni katika usiku uliopambwa na burudani na vinywaji.
 
Kabla ya uzinduzi rasmi wa club hiyo ulioanza saa tano kamili usiku, kulitanguliwa na sherehe maalumu iliyohudhuriwa na wageni 125 waliokaribishwa na Moet na Chandon
Vyumba hivi ni maalumu kwa kuwakutanisha marafiki wanaofurahia jambo fulani au wateja wanaojadili biashara mbalimbali’ alisisitiza bwana Kadri. Club 327 itakuwa ikifunguliwa siku 5 kwa wiki kutoka Jumanne hadi Jumaipili kuanzia saa mbili usiku na kuendelea.
 Kwenye club hii itakuwa ni vyumba vya wageni maalumu vya Moet na Chandon, Hennessy na Belvedere. Vyumba hivyo ambavyo vimeunganishwa na huduma ya DSTV, majokofu yenye vinywaji wakati wote, bafu ya ndani kwa ndani, pamoja na muziki.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster