Wakiongozwa na Rais wa Bendi hiyo kongwe katika tasnia ya
Muziki wa Dansi hapa nchini Nyosh El Sadaat, vijana hao maarufu kama wazee wa Pamba,
walishambulia jukwa la ukumbi huo majira ya nne usiku kwa kuporomosha baadhi ya
nyimbo zao za zamani na nyimbo mbili kutoka katika album mpya ya Chuki ya Nini.
Badhi ya nyimbo zilizopigwa katika shoo hiyo ni pamoja na Vuta
ni kuvute, iliyo kwenye album ya Vuta nikute, Anna, Maisha Kigeugeu kabla ya
kuuteka ukumbi huo uliofurika wapenzi wa muziki wa Dansi kutoka Moshi na Arusha
kwa kucheza Staili yao mpya ya Vundes na nyimbo mpya mbili, Maisha uliotungwa
na Pablo Maasai na wimbo wa Ndoa ya Kisasa uliotungwa na Mulemule.
“Vundes ni Ubunifu na moja ya vitu vikali tuliomua kuwaletea
nah ii ni kuhakikisha wazee wa Ngwasuma, tunayendelea kuwateka na kuwa nambari
wani kwenye muwa dansi, Vundes inamaanisha makalio, ndio maana tunaimba akina
dada wanapenda kucheza vundes na akina kaka wanapenda kuangalia vundes, alisema
Nyoshi
0 COMMENTS:
Post a Comment