Wasanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz'
na Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' usiku wa x-mass waliweka historia kwa
kufanya shoo ya aina yake ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo
Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Wasanii hao walisindikizwa na mkali
Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi, Msanii mkongwe Ally Baucha
pamoja na Bendi ya Extra Bongo. Shoo hii imeletwa kwenu kwa hisani
kubwa ya Serengeti Premium Lager na Vodacom - Wajanja wa Kujirusha.
0 COMMENTS:
Post a Comment