Kampuni ya
Lakeland Africa ya jiji Dar es Salaam imeandaa safari ya kutembelea
hifadhi za taifa na makumbusho ya taifa ili kutoa fursa kwa Watanzania
kusherehekea msimu huu wa Krismas na Mwaka mpya.
Watanzania
wanahamasishwa kujitokeza kushiriki katika safari hiyo ya kitalii ya
siku 14 itakayoanza jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu hadi Desemba 27
mwaka huu. “Kwako mtanzania sasa inawezekana kujua Tanzania yako, si
lazima kuwa mzungu kuwa mtalii wa ndani”
Safari hii
itaanzia Dar es Salaam, na kupita katika hifadhi za Sadan, Pangani,
Lushoto, Tarangire, Ziwa Manyara, Ngorongoro Crater, Hifadhi ya
Serengeti na itahitimishwa Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere.
Safari hii
itatumia magari ya kisasa makubwa yenye uwezo wa kubebe watalii 24 na
kutoa nafasi kutumia vifaa vya umeme (laptop, simu, kamera) kwa kila
mtalii kuwa na soketi yake. Magari ambayo yamekuwa yakitumiwa na
makampuni ya utalii katika nchi za ulaya sasa kutumika Tanzania pia.
Gharama za
safari hii zinajumuisha chakula, malazi, usafiri, tozo za kuingia
hifadhini na tiketi ya ndege kutoka Mwanza kurudi Nyumbani.
Kwa mawasiliano na Lakeland Africa
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako’
0 COMMENTS:
Post a Comment