
Naomba
kushare hii na wadau , Kwa kifupi niko kwenye mahusiano mapya yapata
miezi nane tu, na Jamaa keshanitangazia Ndoa , tatizo linakuja anataka
tufunge Ndoa ya Siri ya Serikalini then baadaye ndiyo tunakuja Bariki
Kanisani , Nikiuliza sababu ni kuwa anajaribu kukwepa Complications za
Kanisa kwa kuwa hana Vyeti vya Ubazito na Wazazi wake woote
walishafariki, Nikimshauri tukajieleze kanisani anakataa , amekazana
hiyo haita kubaliwa tutapoteza muda ni heri tufunge kwanza Serikalini ,
then tuanze na kufuatilia ya Kanisa Taratibu
Nikimpekua pekua simkuti na chochote cha kunioneshea labda anamahusiano na kama anayo basi ni Msiri sana
Mbaya
zaidi hiyo Ndoa ya Serikali hataki wapambe wala kuvaa Shela wala Picha
eti tuende na nguo za kawaida tu kupunguza Bajeti !
heshima
ya Ndoa ninaitaka lakini mbona hii hainiingii, kuna inayemuingia hapa
?Hivi Raha ya Ndoa ni nini si ujumuishe watu ??au nimekutana na JINI
Maana hana Ndugu wengi , zaidi ya Jamaa za hapa na pale
Desperate Woman
Kuwasiliana nasi tuma emailsonramso@yahoo.com
0 COMMENTS:
Post a Comment