Taswira za Baiskeli ya mpitajia mbaye hakujulikana jina lake na jinsi Baiskeli yake ilivyoathiliwa na Katapila hilo.
Wakazi wa Wilaya ya Nyamagana walijitokeza kushuhudia tukio hilo lililoguswa na kila aliyeshuhudia.
Wasamalia wema wakisaidia kumtoa kijana aliyekubwa na mkasa huu chini ya katapila hilo
Baiskeli ya mpita njia ikiwa chini ya Katapila hilo lililotaka kuondoa uhai wa kijana.
Ajali hii imetokea katika Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza eneo la
Igoma, Chanzoi kinasema kuwa Katapila hilo Lilikuwa katika mwendo kasi likitokea Shamaliwa
katika uboreshaji wa Barabara hiyo, Na kisha lilikosea njia na kuingia katika mtalo wa pembeni ya barabara
na ilikuwa ni sehemu yenye kona kali sana, Pembeni ya njia hiyo
kulikuwa na mpitanjia aliyekuwa na Baiskeli akiendesha kuelekea
lilikokuwa likitokea Katapila hilo, Baada ya tukio hilo Dereva wa Katapila hilo alitokomea kusikojulikana akidhania amepoteza uhai wa mpitanjia, aliyekuwa akidhaniwa kuwa na umri usiopungua miaka 25. Ingawa kijana aliyekumbwa na mkasa huo hakupoteza Maisha bali alipata majera kidogo sehemu ya mwili wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment