November 17, 2012

VAN VICKER, MWIGIZAJI ANAYEPIGWA VITA NCHINI NIGERIA HIVI SASA.

Hi | 6:03:00 PM |
Huyu jamaa anaitwa JOSEPH VAN VICKER! Ni mwigizaji maarufu wa Movie za Kinigeria anayejulikana sana Barani Africa! Baba yake ni Mholanzi na mama yake ni Mghana. 
Baba yake alifariki Dunia wakati Van Vicker akiwa na umri wa miaka 6 na kuanzia hapo alilelewa na mama yake mpaka alipokuwa na uwezo wa Kujitegemea! Jamaa ameshanyakuwa Tuzo kibao za Filamu na pia inasemekana baada ya yeye kutoka kwao Ghana na kuhamishia kazi zake za Filamu nchini Nigeria na kukumbana na Ubaguzi mkali kwa wadau wa Filamu na hasa waigizaji wa Nollywood waliodhani aatawafunika na kweli 'AKAWAFUNIKA' kweli na hata waigiza maarufu wa kimume nchini humo kama vile RAMSEY NOAH, JIMMY IYKE na wengineo jasho linawatoka sasa...
Hobbies za huyu jamaa ni kucheza Football, Table tennis na kuogelea
Mwigizaji huyu anayependwa sana na wakina Dada ameshaoa jamani na amejaaliwa kupata watoto 3! Kwaiyo kama kuna siku ulikuwa na ndoto 'MBAYA' na yeye basi imekula kwako

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster