Mtoto Aneth mara baada ya kuunguzwa na kuokolewa na msamaria mwema, Haya ndo majeraha aliyo nayo mtoto Aneth baada ya kuunguzwa na mama yake mdogo.
Mthumiwa wa kumuunguza mtoto Aneth ambaye ni mama yake mdogo anaejulikana kwa jina la Bahati Lukangara
Mthumiwa akiwa amesungukwa na majirani baada ya tukio
Majirani
wakihjaribu kuzungumza na mama mdogo wa Aneth ili kujua sababu za yeye
kuumunguza mtoto huyo, lakini inasemakana hakujibu wala kueleza kitu
chochote
Mwenyekiti
wa mtaa huo Habiba Mwaktalu akiongozana na Diwani wa kata ya Majengo
Mh. Samwelu wakiwa na mtoto Aneth tayari kwa kumpeleka hospitali
Mama mdogo wa Aneth akiwa ameshikiliwa na wananchi wenye hasira kali wakimpleka kituo cha polisi
---
Katika hali isiyo ya Kawaida Mkazi wa majengo jijini Mbeya Ndugu Bahati Rukangara amemchoma moto mtoto mdogo wa mika 3 aliyefahamika kwa jina la Aneth kisha kumfungia Ndani na kumlazimisha ale kinyessi chake.
Akizungumza
Mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Habiba Mwakitabu amesema kuwa tukio
hilo limetokea majira ya saa 10 :30 asabuhi ambapo majirani na mwanamke
huyo waligundua mara baada ya kusikia sauti ya mtoto huyo akilia
kutokana na maumivu.
Amesema
mara baada ya kusikia sauti hiyo walifika eno hilo na kunza kumhoji ili
kufahamu kiini cha tatizo hilo ambapo alishindwa kutoa ushirikiano
ndipo walipo anza kumpiga .
Amesema
kutokana na hali hiyo majirani walilazimika kubomoa mlango ndipo walipo
mkuta mtoto huyo akiwa uchi huku ameungua vibaya mwilini hasa katika
upande mmoja eneo la mkono wa kushoto .
Amesema
mara baada ya kumhoji mtoto huyo aliwaeleza kuwa mama yake mdogo
alichukua nguo na mkumfunga mkononi kisha kumwagia maji ya moto pamoja
na kumlazimisha ale kinyesi chake hali ambayo iliwafanya washindwe
kuvumilia na kuanza kupiga kelele kwa lengo la kuomba msaada kwa watu
wengine.
Kwa
mujibu maelezo ya mwenyekiti huyo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo amekuwa
akifanya vitendo vya manyanyaso kwa mtoto huyo marakwamara ambapo
wamekuwa wakimuonya lakini amekuwa si mtu wa kusikia.
Ameesema
mtoto huyo si wa kwa kwakwe kwani amekuwa akiishi naye kwa muda mrefu
sasa ambapo aliachiwa na dada yake ambaye hakufahamika kuwa nayishi wapi
kwa sasa.
Hata
Diwani wa kata hiyo Ndugu Samuel Mamboma alifika eneo hilo tukio na
kutoa msaada wa usafiri kwa lengo la kumfikisha mama huyo polisi pamoja
na mtoto huyo ambaye naye alikimbizwa Hospitali.
Hata
hivyo amesema tukio hilo si la kwanza kutokea katika meaeno hayo kwani
kumekuwepo na matukio mengi hasa ya utoaji mimba na kutupwa watoto.
0 COMMENTS:
Post a Comment