Vurugu kubwa zimetokea mchana huu maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, ambapo baadhi ya Waislamu wanaandamana kuelekea Kidongo Chekundu. Polisi wanatumia mabomu ya machozi kutawanya mikusanyiko ya watu waliokuwa wamejiandaa kuandaamana kuelekea Ikulu ya Magogoni jijini. Hali imekuwa tete na polisi wamelazimika kutumia helikopta kuzuia vurugu.
Maduka yote katika maeneo hayo yamefungwa na shughuli mbalimbali zimesimama pamoja na Ofisi mbalimbali zimefungwa kutokana na hofu kubwa iliyotanda. Pia inasemekana maeneo ya Kinondoni, napo kimenuka, Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kinapambana na Wailslamu kutoka msikiti wa Mkwajuni.
Kwa mujibu wa Francis Dande blog, Redio One imetangaza kwamba wananchi wanakimbizana hovyo kukimbia mabomu ya machozi yaliyokuwa yakipigwa na Polisi kuwatawanya waumini waliokuwa wakitoka msikitini.
Picha ya bango, kutoka http://wavuti.com, iliyosambazwa kuhamasisha maandamano.

0 COMMENTS:
Post a Comment