Siku moja baada ya kamati iliyoundwa
na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuchunguza
mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari mwakilishi wa kituo cha
televisheni ya Channel Ten, mkoani Iringa, marehemu Daudi Mwangosi,
kutoa ripoti yenye ‘makengeza’ kuhusu Jeshi la Polisi, Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora imejiridhisha kuwa jeshi hilo lilivunja haki za
binadamu, ikiwamo Kamanda wake wa Mkoa huo, Michael Kamuhanda, kukiuka
misingi ya utawala bora, katika kuendesha operesheni iliyosababisha
mauaji ya mwanahabari huyo, kinyume cha Katiba na sheria za nchi.
0 COMMENTS:
Post a Comment