October 14, 2012

TASWIRA ZA MSIBA NYUMBANI KWA MAREHEMU SACP LIBERATUS BARLOW

Hi | 6:45:00 PM | | |
Nyumba ya Dorcas Moses mwalimu wa shule ya Msingi ya Nyamagana ambaye alikuwa kwenye gari aina ya Rav 4 aliyopewa lifti na kamanda Ballow usiku kumrudisha kwake. Hapa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Fredrick Katulanda akitoka kufanya mahojiano.
Mtoto wa kaka yake Mwalimu Dorcas akiongea kuhusiana na tukio la Kifo cha kamanda Ballow ambapo yeye ndie alikwenda kufungua geti kwa ajili ya Mama yake Dorcas aweze kuingia ndani ila kabla ya kufungua ndipo aliposikia risasi ikipigwa.
Hili ndilo geti ambapo kifo cha kamanda Ballow kilipotokea usiku wa kuamkia leo wakati mwalimu Dorcas Moses alipokuwa akirudi nyumbani kwa lifti ya gari la Kamanda Ballow.
Waombolezaji wa kike wakilia kwa uchungu nyumbani kwa kamanda Ballow

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster