Watu nane wenye silaha wameteka basi la Sumry baada ya kuweka kizuizi cha magogo na mawe katika msitu wa Msaginya ulioko katika Mkoa wa Katavi, maeneo ya barabara kuu ya Sumbawanga – Mpanda.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, amesema uhalifu huo ulifanyika saa sita usiku wa kuamkia jana wakati basi hilo, usajili T107 BHT, likisafiri kutoka Sumbawanga kuelekea Mpanda.
Alifafanua kwamba dereva alilazimika kusimamisha basi baada ya kukumbana na vizuizi hivyo, basi lilipofika eneo hilo lenye mteremko na kona kali. Inadaiwa kwamba watu nane waliibuka kutoka mafichoni wakiwa na silaha za jadi zikiwamo mapanga, nondo, mawe na visu na kuwalazimisha abiria wote kushuka. Waliwapekua na kuwapora abiria hao simu za mkononi 15 na kiwango kikubwa cha fedha.
Taarifa nyingine kutoka eneo hilo inadai kwamba baadhi ya abiria walivuliwa nguo wakati wa upekuzi huo na na abiria wote kulazimishwa kulala chini.

0 COMMENTS:
Post a Comment