November 1, 2011

MOTO WA REDD’S UNI – FASHION BASH 2011 VYUO VYA DAR ES SALAAM WASHINDI WAPATIKANA

Hi | 4:49:00 PM |
 Meneja Uhusiano wa TBL,Edith Mushi akimkabidhi zawadi msindi wa kwanza wa Mitindo katika Tamasha la Redd’s Uni-Fashion Bash,Marvin Peter.

Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original,Victoria Kimaro akikabidhi zawadi ya mshindi wa Kwanza wa Ubunifu,Jackson gumbala (Udsm).

Kinywaji cha Redd’s Original kinachotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kesho kitafanya tamasha lake la kwanza kwa wabunifu na wanamitindo wa vyuo vya Dar es Salaam. Tamasha hili lijulikanalo kama “Redd’s Uni-Fashion Bash” lilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi October likiwa na lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya wabunifu na wanamitindo walioko katika vyuo vya elimu ya juu.

Tamasha la fainali za jana zilikuwa na mvuto wa kipekee na lenye mvuto mkubwa, Ambapo washiriki walifanikiwa kuonyesha ubunifu mkubwa na umahiri wa hali ya juu tofauti na matarajio ya walio. Fainali za tamasha la Redd’s Uni – Fashion Bash kwa vyuo wa Dar es Salaam lilifanyika katika ukumbi wa FPA Uliopo chuo kikuu cha Dar Es Salaa karibu na Benk ya CRDB (Udsm) hapa Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni na kumalizika usiku wa manane.

Tamasha limeonekana kuwa na maandalizi makubwa kuanzia kwa majaji ambapo waliweza kutoa vigezo mbalimbali na namna wabunifu na wanamitindo wanapaswa kuwa.

Washindi katika tamasha la jana

a)Mitindo

1.marvin peter (Ustawi wa jamii)
2.Benson Macha(Cbe)
3.Asha Mohamed (TIU)
4.Yusuph Fanuel (Cbe)
5.Aloycia Innocent (Udsm)

Ubunifu ni

1.Jackson gumbala (Udsm)
2.Esther Amos(Cbe)
3.Mirium kairus(IFM)
4.Shabani (Udsm)

Ambapo waliweza kukabidhiwa zawadi zao pale pale ukumbini toka kwa wadhamini wa shindano hilo kampuni ya bia nchini Tbl kupitia kinywaji chake cha Redds Original.

Aidha shindano hilo lilikuwa na burudani mbalimbali zilizoandaliwa na Redd’s Original ambapo wasanii Roma Mkatoliki na John Makini walitoa burudani ya kutosha.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster