June 27, 2011

Ajali za kila siku na SunLG

Hi | 11:40:00 AM |
Ajali zimekuwa zikiongezeka tangu ianze hii biashara ya tukutuku Jijini Mwanza, Ikiwa wengi wao hupendelea kutumia Pikipiki aina ya SunLG kwani ndizo zilizokuja kwa wingi sana kupelekea kila mtu kuhitaji kuwa na ka chombo ka usafiri wengine kwa matumizi yao binafsi na wengine kama biashara, Mpaka sasa Hospitali ya Bugando imeandaa Wodi inayoitwa SunLG kwani wamekuwa wakipokea wagonjwa wengi sana kwa siku, Pia tumekuwa tukipata taarifa mbali mbali ambazo hutangazwa au hulipotiwa kwenye vyombo vya habari kila kunapokucha juu ya ajali za pikipiki kila pande, Hivyo hali hii inatisha na inapunguza vijana ambao ni tegemezi na ni Taifa la Leo, Ki ukweli ni usafiri ambao huwaisha na ni wa haraka kupita kiasi tofauti na Hiace au Tax, Ila tujihadhali na kuwa makini kwa wale waendesha Tukutuku kwa ujumla kwani chanzo chake huanzia kwao nikiwa na maana ya kuwa hawana elimu ya kutosha na mafunzo ya muda mrefu, Hivyo ikiwa kama ombi langu kwa Serikali ili kunusuru maisha ya vijana na wazazi naomba madereva wote wa Tukutuku wapewe semina na watambue haki zao za msingi na hasa wanapokuwa barabarani kwani wengi wao hawajui Sheria zao hasa wakiwa katika barabara.
Kama unavyoona pichani hii ni ajali ya Tukutuku iliyotokea hivi karibu Jijini.

0 COMMENTS:

Home of Technologies © Copyright 2010-2015 : Designed by : WebMaster